Home KILIMOKILIMO BIASHARA Waziri Bashe akabidhi hundi ya bilioni 13 kwa wakulima wa tumbaku

Waziri Bashe akabidhi hundi ya bilioni 13 kwa wakulima wa tumbaku

0 comment 12 views

Waziri wa Kilimo,  Hussein Bashe amekabidhi hundi ya Shilingi Bilioni 13 kwa Chama cha Ushirika cha Tobacco Cooperative Joint Enterprises Limited (TCJE) kwa ajili ya malipo ya ruzuku kwa wakulima wa Tumbaku nchini.

Waziri Bashe amesema sababu ya Serikali kuwapa wakulima wa Tumbaku fedha hizo ni kwa ajili ya kulipia ruzuku ya zao hilo ili kupunguza gharama za uzalishaji. Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Kilimo, jijini Dodoma 29 Januari 2025.

Ameeleza kuwa Serikali imefanya mageuzi makubwa katika zao la Tumbaku na kupelekea pato la mkulima kuongezeka kutoka wastani wa Dola 1 ya Marekani mpaka kufika Dola za Marekani 2.3, ambapo uzalishaji wa zao hilo unaendelea kuimarika na bei ya mkulima inaendelea kuimarika kutoka wastani wa uzalishaji wa Tani zisizozidi 50,000 mpaka kufika wastani wa Tani 122,000.

Ongezeko hilo limepelekea mapato ya mkulima kuongezeka kufika Dola za Marekani Milioni 269 na mauzo ya nje kufika Dola za Marekani Milioni 484, na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya pili kwenye uzalishaji wa Tumbaku baada ya Zimbambwe na kwa mara ya kwanza mauzo ya nje ya Tumbaku yamefika zaidi ya Dola za Marekani Milioni 400.

Aidha, Bashe amezungumzia matumizi ya mbolea nchini na kusema kabla ya mfumo wa ruzuku ya mbolea kuanza, Tanzania ilikuwa inatumia Tani 360,000 na baada ya kuanza mfumo huo katika msimu wa kilimo uliopita imetumia jumla ya Tani 840,000.

Lengo la Serikali ya Tanzania kwa msimu huu matumizi ya mbolea yaongezeke kutoka wastani wa Tani 840,000 hadi kufika Tani 1,000,000. Matumizi ya mbolea kwa ekari yamepanda kutoka kilo 15 hadi kufika kilo 24 kwa mwaka jana na lengo ni kufika kilo 50 ifikapo 2030.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter