Home KILIMO Kilimo cha michikichi kupigwa msasa

Kilimo cha michikichi kupigwa msasa

0 comment 188 views

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amezindua kampeni inayolenga kufufua michikichi mkoani Kigoma na kuagiza Chuo cha Maendeleo ya Jamii cha Kihinga kuanzisha kituo cha utafiti wa zao hilo. Majaliwa ameeleza kuwa serikali imejipanga kutatua changamoto ya upatikanaji wa mafuta ya kupikia nchini kwa kuhamasisha kilimo hicho kwani takribani Sh. 600 bilioni hutumika kwa mwaka kuagiza mafuta nje ya nchi japokuwa uwezo wa kulima michikichi na kuzalisha mafuta upo.

Katika uzinduzi wa kampeni hiyo, Waziri Mkuu pia ameitaka Wizara ya Kilimo kuanzisha utaratibu wa kisheria kuhamasisha Chuo cha Kihinga kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kufika wizarani ili shughuli za utafiti wa zao la michikichi lifanyike kwa ufanisi.

Majaliwa ametoa wito kwa wadau wa kilimo hicho mkoani Kigoma na mikoa mingine kupanda kwa wingi ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo.

Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Emmanuel Maganga amepongeza uamuzi wa serikali na kufufua kilimo hicho na kusema kuwa, kufanya hivyo kutasaidia kuinua uchumi wa taifa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter