Home KILIMO Malipo korosho yapelekea kusitishwa shughuli AMCOS

Malipo korosho yapelekea kusitishwa shughuli AMCOS

0 comment 92 views

Kufuatia kicheleweshwa kulipwa fedha za ushuru, Vyama vya  msingi vya ushirika (AMCOS) mkoani Mtwara vimesitisha shughuli za ushirika kutokana na kutokuwa na fedha za kuendesha shughuli zao. Wakizungumza mwishoni mwa wiki, iliyopita viongozi wa vyama hivyo kutoka wilaya tano mkoani humo wamesema ushuru huo wa Sh. 70 kwa kilo moja ya korosho hutumika kuendesha shughuli za vyama hivyo kukosekana kwa malipo hayo mapema kumepelekea vyama kushindwa kujiendesha.

Aidha, serikali imeanza kutoa fedha kwa ajili ya kuwalipa makatibu, makarani waliokuwa wanapokea korosho kwenye vyama hivyo na wachukuzi waliopakia magunia ya korosho kutoka kwenye vyama hivyo kwenda kwenye maghala. Matumizi mengine kama vifaa vya ofisini, makatibu waliotumia pesa zao kwenda vijijini kwa ajili ya uhakiki na wajumbe waliokuwa wanasindikiza magari ya korosho kwenda kwenye maghala bado hayajafanyiwa malipo.

Kufuatia maelekezo hayo, viongozi wa vyama hivyo wameshindwa kuwalipa watu hao kuondokana na lawama kutoka kwa wale ambao fedha zao bado hazijaingizwa kwenye akaunti. Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu waWizara ya  Kilimo Prof. Zizah Tumbo amesema malalamiko hayo ameshayawasilisha wizarani ili yafanyiwe kazi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter