Home BIASHARA Mkonge wawakuna wakulima Tanga

Mkonge wawakuna wakulima Tanga

0 comment 122 views

Mkataba mpya uliosainiwa baina ya wakulima wa katani wilayani korogwe na kampuni ya katani ltd umewafurahisha wakulima kufuatia kuwa na maslahi na kuwapa mwanga na mafanikio katika maisha yao.

Mkataba huo uliosainiwa desemba mwaka jana baina ya wakulima hao zaidi ya 200 wenye mashamba matano na kampuni hiyo umewaruhusu wakulima kuuza mazao yao kwa mkulima yeyote mwenye maslahi kwao tofauti na mkataba wa awali ambao wangeuza kwa mfanyabiashara mmoja pekee jambo ambalo liliwanyima fursa ya kuwa na soko pana na lenye tija kwao.

Mmoja wa wakulima na mweyekiti wa shamba la magunga Eliamini Mrutu alisema mkataba mpya utawawezesha wakulima kunufaika na kilimo tofauti na wa awali uliokuwa ukiwabana na kuwanyima fursa ya kuuza kwa faida zaidi.

Licha ya kushuhudia utiaji saini wa mkataba huo,mkuu wa mkoa wa tanga Martin Shigela alibainisha kwamba mkataba wa awali ulikua umepitwa na wakati na kuwa chanzo cha migogoro hivyo aliwasihi wakulima kulima kwa wingi huku akiwakaribisha wafanyabiashara wengine kujitokeza kununua mkonge ili kuleta ushindani wa kibiashara.

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya katani Ltd Juma Shamte alisema lengo la kufikia hatua hiyo ni kujali maslahi ya wote baina ya kampuni na wakulima.

Katani ni moja ya mazao ya biashara yanayolimwa nchini Tanzania hasa mkoani tanga ambapo kuna mashamba tofauti tofauti kama Magoma,Mgombezi,Hale,Mwelya na Magunga.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter