Home VIWANDA Jafo akerwa na mikoa iliyoshindwa kufikia malengo viwanda

Jafo akerwa na mikoa iliyoshindwa kufikia malengo viwanda

0 comment 109 views

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),  Selemani Jafo ameagiza mikoa ambayo imeshindwa kutimiza lengo la ujenzi wa viwanda 100 kila mkoa kuhakikisha inafanya hivyo hadi kufikia Juni mwaka huu. Waziri Jafo amesema hayo wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa mpango huo kwa kila mkoa ambapo ameeleza kutofurahishwa na hali hiyo.

“Sijafurahishwa na mikoa hiyo na inajijua haijafikia malengo ya ujenzi wa viwanda 100 nawapa muda hadi mwezi wa sita mwaka huu, mhakikishe mmefikia malengo mliyowekewa, sitaitaja nimetumia busara za uongozi ingawa kiukweli sijafurahishwa sana, mkishindwa kufikia lengo nitawataja hadharani”. Amesema Jafo.

Waziri huyo amesema ujenzi wa viwanda 100 kila mkoa ni utekelezaji wa mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano (2016/2017-2020/2021) ambao umejikita zaidi katika ujenzi wa uchumi wa viwanda. Imeelezwa kuwa hadi Desemba mwaka jana, takribani viwanda 4,777 vilikuwa vimejengwa nchi nzima, ikiwa ni sawa na asilimia 183.73 ya lengo licha ya kwamba baadhi ya mikoa imeshindwa kutekeleza ujenzi huo.

Jafo ametaja mkoa wa Dar es salaam kuwa minara wa ujenzi wa viwanda ukifuatiwa na Pwani, Mwanza, Lindi na Simiyu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter