Home VIWANDA Kigwangalla apigania uchumi wa viwanda

Kigwangalla apigania uchumi wa viwanda

0 comment 108 views

Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla ameagiza Mfuko wa Ruzuku wa Misitu Tanzania (TAFF) pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kufanya kazi pamoja na kuanzisha mradi wa viwanda vidogo vya usindikaji na kufungasha asali katika mikoa ya Katavi na Tabora.

Dk. Kigwangalla amefafanua kuwa lengo la kufanya hivyo ni kuongeza uzalishaji wa zao la tumbaku na kujenga uchumi wa viwanda kwani asilimia kubwa ya wakazi wa mikoa hiyo hutegemea kilimo cha tumbaku kuendesha maisha yao japokuwa mazingira sio rafiki kufanya kilimo hicho.

“Tuwawezesha wananchi wajiunge katika vikundi, tuwagawie mizinga ya kisasa, wafuge nyuki kisasa, warine asali kisasa, wakisharina wapeleke kwenye viwanda, ifungashwe kisasa, ipate bei kubwa, na mwisho wa siku wataona faida ya kuwa na misitu”. Amesema Dk. Kigwangalla.

Waziri huyo pia amewashauri wananchi katika mikoa hiyo kujikita katika kilimo cha korosho kama njia nyingine ya kuongeza kipato chao badala ya kutegemea kilimo cha tumbaku pekee ambacho kwa kiasi kikubwa kinasababisha uharibifu wa misitu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter