Home VIWANDA Majaliwa azindua Mwongozo wa Viwanda

Majaliwa azindua Mwongozo wa Viwanda

0 comment 125 views

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezindua Mwongozo wa Kusimamia Ujenzi wa Maendeleo ya Viwanda kwa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Majaliwa amezindua mwongozo huo wakati akizindua maonyesho ya mwaka huu ya Sabasaba ambapo ameeleza kuwa, kupitia mwongozo huo, jamii itapata fursa ya kujifunza umuhimu wa kuanzisha viwanda.

Mwongozo huo unafafanua taratibu za kuanzisha ujenzi wa viwanda, uchumi pamoja na uelewa wa pamoja. Vilevile kupitia mwongozo huo, wananchi watapata fursa ya elimu kutokana na kwamba, mwongozo huo utawezesha majukwaa ya kibiashara na kiuchumi ndani ya jamii.

Waziri Mkuu amedai kuwa, uwepo wa mwongozo huo utasaidia wananchi na kuongeza hamasa ya kujenga viwanda, hali ambayo itaenda sambamba na mpango wa pili wa serikali wa maendeleo ya kujenga viwanda kwa kutumia malighafi zinazozalishwa na watanzania wenyewe.

Mbali na hayo, Majaliwa pia alipata fursa ya kuzindua mradi wa matrekta 2,400 yaliyounganishwa na kampuni ya URSUS ya nchini Poland kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC). Mradi huo unalenga kuwainua wakulima na kuongeza uzalishaji wa mazao.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter