Home VIWANDAMIUNDOMBINU Flyover Tazara yazinduliwa rasmi

Flyover Tazara yazinduliwa rasmi

0 comment 107 views

Uzinduzi wa daraja la juu (Flyover) Mfugale eneo la Tazara jijini Dar es salaam unafanyika siku ya leo ambapo Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli ataongoza tukio hilo la kihistoria, ikiwa barabara hiyo ni ya kwanza katika historia ya nchi. Viongozi wengine katika uzinduzi huo ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Seleman Kasoso, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Tizeba na Mwakilishi wa Shirika la JICA Toshio Nagase.

Ujenzi wa Flyover hiyo uliogharimu Dola za Marekani Sh. 45 milioni (takribani bilioni 100 za kitanzania) ulianza mwezi Oktoba 2016, kwa udhamini kamili wa serikali ya Japan na barabara hiyo ilifunguliwa tangu Septemba 15 ili kuruhusu madereva kuifanyia majaribio kuelekea uzinduzi wake rasmi leo. Barabara hiyo inatazamwa kuwa suluhisho mojawapo la kupunguza tatizo la muda mrefu la msongamano na foleni katika eneo hilo na kuongeza muda wa watu kufanya kazi badala ya kupoteza muda mwingi barabarani.

Hadi kufikia sasa, mamia ya wananchi tayari wameshawasili eneo la tukio kushuhudia sherehe za uzinduzi huo. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (Tanroads) Patrick Mfugale amesema wakati wa mahojiano maalum na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kuwa, barabara hiyo imejengwa ili kupunguza foleni iliyokuwa ikichelewesha harakati mbalimbali za kiuchumi.

“Hii ni Flyover kwa sababu imepita juu ya barabara nyingine na tumeweza kupunguza foleni kwa asilimia 100 kwa wale wanaotoka mjini kwenda uwanja wa ndege na wale wanaoelekea mjini kutoka Gongo la mboto”.Amesema Mfugale ambaye daraja hilo limepewa jina lake.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter