Home FEDHAMIKOPO Deni la taifa laongezeka

Deni la taifa laongezeka

0 comment 64 views

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amesema deni la taifa kwa mwaka 2018 limefikia Sh. 49.37 trilioni, ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 3.2 ikilinganishwa na Septemba 2017 ambapo deni hilo lilikuwa Sh. 47.82 trilioni. Waziri Mpango amesema hayo wakati akitoa taarifa ya fedha ya hali ya uchumi wa taifa na utekelezaji wa bajeti ya serikali ya nusu mwaka ya 2018/2019 jijini Dodoma.

“Nchi kuwa na deni sio dhambi, jambo muhimu ni kuhakikisha kuwa fedha tulizokopa zinatumika kujenga rasilimali ambazo ni msingi wa kuongeza uwezo wetu wa kuzalisha mali na kulipa mikopo hiyo”. Amesema Dk. Mpango.

Dk. Mpango ameeleza kuwa katika deni hilo, la ndani ni Sh. 13.64 trilioni sawa na la nje ni Sh. 35.72 trilioni huku akitaja sababu za deni hilo kuwa ni mikopo kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es salaam, ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, madaraja na bandari.

Miradi mingine ni ujenzi wa mitambo ya kufua umeme ya Ubungo, Mwanza na Kinyerezi II, miradi ya maji ikijumuisha wa maji wa Ziwa Victoria. Vilevile miradi ya Tasaf, mkongo wa taifa wa mawasiliano pamoja na mradi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA). Aidha, Dk. Mpango amesema kwa mujibu wa matokeo ya awali ya tathmini iliyofanywa Desemba mwaka huu, deni hilo ni himilivu kwa muda mfupi na mrefu.

Waziri huyo amesema serikali itaendelea kusimamia deni na kuhakikisha linaendelea kuwa himilivu huku mikopo ikielekezwa katika miradi ya maendeleo na ambayo inachochochea ukuaji wa uchumi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter