Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu amesema Serikali imeamua kukataa gawio la Sh 109 bilioni lililotolewa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).
Mchechu amesema hayo katika uzinduzi wa taarifa ya mwaka wa fedha 2021/2022 na Mapango mkakati wa Shirika wa miaka kumi.
Amesema serikali imeachia Shirika hilo fedha hizo ili zitumike katika kupanua miradi ya umeme nchini.
“Tunataka gawio hilo litumike kama mtaji wa kuimarisha utoaji wa huduma zao,” amesema Mchechu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Maharage Chande amesema mwaka 2021/2022 shirika hilo limepata faida ya Sh109 bilioni huku akizitaja fedha hizo zitatumika katika kuwaunganishia umeme wateja wengine.