Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani amesema nishati ya umeme ni muhimu kwa ajili ya uzalishaji viwandani hivyo serikali itahakikisha tatizo la umeme kukatika kwenye viwanda linadhibitiwa kwani hali hiyo sio salama viwandani. Dk. Kalemani amesema pamoja na changamoto hiyo, anawataka wawekezaji kuendelea kujenga viwanda kwani kuna umeme wa kutosha, ikiwa hivi sasa kuna akiba ya umeme wa ziada wa megawati 148. Waziri huyo amesema hayo mjini Kibaha alipotembelea maonyesho ya viwanda yanayofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba ambapo ametumia fursa hiyo na kulielekeza Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) kutangaza vituo vya gesi asilia ili wananchi wafahamu zaidi kuhusu gesi hiyo.
140