Na Mwandishi wetu
Meneja wa Shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo (SIDO) Mkoa wa Kilimanjaro Hamweli Meena amesema kuwa ugunduzi wa teknolojia ya mashine za kisasa za kusaga chupa za plastiki na kubadili taka kuwa malighafi kwa viwanda hapa nchini itazalisha ajira za ukusanyaji wa chupa za plastiki na hivyo kuongeza idadi ya viwanda vidogo.
Arthur Ndedya, Meneja wa kitengo cha TDC ambacho husimamia Maendeleo ya teknolojia akielezea kwa undani juu ya ugunduzi huo amesema gharama za mashine moja inafikia zaidi ya Sh 4.5 milioni hivyo wajasiriamali wadogo wanaweza kununua na kuzitumia ili kujiajiri.
Mbali na hayo, Meya wa Manispaa ya Moshi, Raymond Mboya amesema kuwa teknolojia hiyo mbali na kuwezesha wananchi kwenye masuala ya ujasiriamali, itasaidia kudumisha usafi katika manispaa hiyo.
Katika mashindano ya usafi wa mazingira kwa mwaka 2017 ambayo yalishirikisha halmashauri 185 yakiwemo majiji manne, manispaa ishirini na moja, miji ishirini na moja na halmashauri za wilaya ishirini na saba Manispaa ya Moshi iliibuka kidedea kwa kupata asilimia 78.5