Home VIWANDA Teknolojia ziendane na mazingira halisi-Ole Nasha

Teknolojia ziendane na mazingira halisi-Ole Nasha

0 comment 119 views

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha, kuelekea Tanzania ya viwanda, kuna umuhimu kwa wabunifu nchini kubuni teknolojia zinazoendana na mazingira halisi ya nchi. Naibu huyo amesema hayo wakati akizindua wiki ya ubunifu jijini Dar es salaam na kuongeza:

“Kwa nchi yeyote ambayo inaendelea, hauwezi kuendelea, kiendelevu kama hauna teknolojia ambayo inatoka kwako, ambayo inaendana na mazingira halisi ya nchi yako. Kwa hiyo ndio maana tunataka watanzania wawe wabunifu, waweze kubuni bidhaa na teknolojia ambazo zitatusaidia kama nchi”. Amesema.

Naibu Waziri huyo amesema serikali inafanya jitihada kubwa kuwasaidia wabunifu kuendeleza ubunifu wao kwa kufanikisha bidhaa zao kuingia sokoni na kuandaa mashindano ya kitaifa ya sayansi na teknolojia ambapo washindi hupewa ufadhili ili kuendeleza kazi zao kwa ajili ya matumizi.

“Na ndiyo maana pia tunatumia wiki hii kusaidia kuwaleta wabunifu mbalimbali kuonyesha kazi yao, lengo ni kuona namna gani wanaweza kusaidiwa ili ziweze kutumika. Sayansi, teknolojia na ubunifu ni vitu ambavyo vinabadilika kwa haraka sana, sera yetu tumeibadilisha ili iendane na mazingira ya sasa, lakini ituongoze namna ya kuwatambua wabunifu na kuendeleza kazi zao. Tumefika hatua nzuri na hivi karibuni tunatarajia kwamba itafika katika Baraza la Mawaziri na hatimaye kupitishwa kwa matumizi”. Amesema Ole Nasha.

Wiki ya ubunifu imeandaliwa na Mfuko wa Ubunifu kwa Maendeleo ya Binadamu (HDIF) pamoja na Tume ya Taifa ya Sayanzi na Teknolojia (COSTECH) kwa ufadhili wa serikali ya Uingereza.

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter