Home VIWANDA Wenye viwanda vya chuma waomba serikali kuwalinda

Wenye viwanda vya chuma waomba serikali kuwalinda

0 comment 125 views

Mwenyekiti wa wamiliki wa viwanda vya chuma Lawrence Manyama ametoa wito kwa serikali kwa niaba ya wazalishaji wa bidhaa za chuma kudhibiti nondo ambazo zipo chini ya kiwango ili kulinda  viwanda vya ndani vya bidhaa hiyo. Manyama amesema hayo wakati wa mkutano na Tume ya Ushindani (FCC) ambapo alieleza kuwa japokuwa viwanda vya ndani havizalishi kwa asilimia mia moja, vinapaswa kulindwa.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, takribani nondo tani 600,000 huzalishwa nchini huku mahitaji yakikadiriwa kuwa ni tani 700,000. Akizungumzia suala hili, Katibu Mkuu wa wizara ambaye anashughulikia masuala ya viwanda Ludovick  Nduhiye amesema watalifanyia uchunguzi suala hili kwa undani zaidi.

Kwa upande wake, John Mduma ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa FCC amesema kuwa wamekuwa wakiendelea kutoa elimu katika jamii kuhusu namna ambazo unaweza kutambua bidhaa feki na kuyafikisha malalamiko yao mahali husika ili sheria ichukue mkondo wake.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter