Home BIASHARA Faida 3 za kufanya biashara na ndugu

Faida 3 za kufanya biashara na ndugu

0 comment 119 views

Watu wengi wamekuwa wakisisitiza kuwa kuanzisha biashara na ndugu au marafiki sio wazo zuri na mara nyingi huishia kwenye ugomvi lakini wakati mwingine, kufanya biashara kwa kushirikiana na watu wako wa karibu zaidi ni nguzo ya mafanikio. Japokuwa ni kweli kuwa biashara nyingi za aina hii zimeshindwa kutimiza malengo, hatuwezi kukataa kuwa ndugu/marafiki huwa na mchango mkubwa zaidi ambao ni vigumu kupatikana kwa watu ambao huna mahusiano nao.

Hapo chini ni faida kubwa tatu (3) za kuanzisha biashara na familia au watu wako wa karibu.

Uaminifu

Hakuna kitu muhimu katika biashara kama uaminifu. Unapofanya biashara na ndugu au hata rafiki, una uhakika kuwa biashara yako ipo katika mikono salama na hii huepusha migogoro ya mara kwa mara ambayo wakati mwingine hudidimiza maendeleo ya biashara. Utamuamini nani kama unavyomuamini ndugu yako? Kila biashara huhitaji uangalizi wa karibu na huwezi kufanya kila kitu peke yako. Endapo ukiwa na msaada kutoka kwa ndugu au marafiki, unakuwa na amani hata kama haupo eneo la kazi kwani una uhakika kuwa kila kitu kinakwenda sawa kama inavyotakiwa kwa kuwa unamuamini uliyemuacha kwa asilimia zote.

Mawasiliano mazuri

Mara nyingi wafanyabiashara wanagombana kutokana na kutofautiana mawazo au kushindwa kuelewana. Unaweza kuepuka hili kama ukifanya biashara pamoja na familia au marafiki zako wa karibu kwa kuwa mnafahamiana vizuri hivyo mawasiliano yenu yatakuwa mazuri zaidi. Mawasiliano mazuri ni muhimu sana katika mafanikio ya biashara na sio rahisi kwa ndugu kushindwa kuelewana na kujenga mahusiano mazuri siku zote. Mnapokuwa na mahusiano imara, mnajenga msingi ya mawasiliano mazuri na inakuwa rahisi kuzungumza kuhusu kitu kwa uwazi sababu ya ukaribu wenu ambao unaenda nje ya masuala ya biashara.

Malengo yanayoendana

Biashara inapokuwa na watu wengi nyuma yake, ni kawaida kwa malengo kupishana na kila mtu kuona malengo yake binafsi yana umuhimu zaidi kuliko ya watu wengine. Unaposhirikiana na familia au marafiki wa karibu, tayari unafahamu ni watu wa aina unawaleta katika biashara. Unapoamua kufanya knao kazi, sababu mojawapo ya uamuzi huo ni kwamba malengo yenu yanaendana hivyo wote mtawekeza jitihada za kutosha kutimiza malengo hayo kwa pamoja.

Wakati mwingine unachohitaji kufanikiwa katika biashara na vitu vingine vingi katika maisha ni ushirikiano kutoka kwa familia na watu wa karibu. Kama unafikiria kuanzisha biashara na ndugu au marafiki, usisite kufanya hivyo ikiwa mawazo na malengo yenu yanaendana. Ni kweli kwamba wakati mwingine biashara haziendelei lakini hii isikukatishe tamaa. Ikiwa wote mpo tayari kufanya kazi kwa bidii, basi bila shaka malengo yeny yatatimia.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter