Home VIWANDA SIDO kusimamia uanzishwaji wa viwanda kila wilaya

SIDO kusimamia uanzishwaji wa viwanda kila wilaya

0 comment 112 views
Na Mwandishi wetu

Shirika la Kuhudumua Viwanda Vidogo (SIDO) limekuwa likihamasisha viongozi wa wilaya zote nchini kuchangamkia Mkakati wa wilaya moja bidhaa moja (ODOP) ili kuongeza ajira na uzalishaji ambayo itapelekea azma ya Tanzania ya viwanda kutimia. Mkurugenzi Mkuu wa SIDO, Prof. Sylvester Mpanduji amesema shirika hilo limeanzishwa ili kuendeleza viwanda vidogo kote nchini hivyo watasimamia mkakati huu na kuhakikisha unafanikiwa.

Prof. Mpanduji amesema mkakati huu waliouanzisha mwaka 2007 una nia ya kuhamasisha wilaya kutumia rasilimali zinazowazunguka na kuanzisha viwanda kwani Tanzania ina ardhi nzuri ya kilimo na kila wilaya ina zao linalostawi vizuri hivyo ameshauri wananchi kushirikiana na serikali na taasisi zisizo za kiserikali ili kupata mavuno ya hali ya juu na kuwezesha uwepo wa viwanda vidogo kote nchini.

Mkurugenzi wa Mafunzo na Huduma za Mikoa SIDO, Joyce Meru amesema wananchi wanapaswa kuchangamkia fursa huku akishauri viongozi wa wilay kuchagua mazao ambayo wanaona yanafaa katika maeneo yao. Meru ameongeza kuwa kufanya hivi kutapunguza idadi ya vijana wanaokimbilia mijini ambako ajira zimekuwa ngumu kupatikana.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter