Home KILIMO Serikali yawatoa hofu wakulima wa korosho

Serikali yawatoa hofu wakulima wa korosho

0 comment 41 views

Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchwaishaija amesema ili kuhakikisha azma ya serikali ya kununua korosho yote ya wakulima inatimia, uongozi wa wizara hiyo unawahakikishia wakulima wote wa mikoa ya kusini kuwa, serikali imejipanga kununua na kuhifadhi korosho yote. Prof. Buchwaishaija amesema hayo wakati akihitimisha siku ya kwanza ya operesheni ya ukaguzi wa maghala katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

“Ziara ya ukaguzi wa maghala inatokana maagizo ya kikao cha tathmini ya operesheni korosho kilichoitishwa na Mwenyekiti wake Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga, ambapo pamoja na mambo mengine kilibaini ufinyu wa maeneo ya kuhifadhia korosho kutoka kwa wakulima”. Amesema Prof. Buchweishaija.

Katika ziara hiyo ambayo Katibu huyo aliongozana na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo pamoja na maafisa wengine, walifanikiwa kukagua maghala ya korosho wilayani Mtwara, Mtama, Masasi na Nachingwea na kugundua kuwa maghala makuu na yale ya uhifadhi yana nafasi ya ziada kuhifadhi korosho zaidi ya tani elfu arobaini na nane.

“Nachukua nafasi hii kuwatoa wasiwasi wakulima wote kwamba, maghala na sehemu za kuhifadhi korosho zetu sio tatizo tena, na tutahakikisha korosho zote ziliyopo kwenye AMCOS (vyama vya msingi) tunazisafirisha haraka iwezekanavyo kabla ya msimu wa mvua kuanza.” Amesisitiza Katibu Mkuu huyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter