123
Kiwanda kidogo cha mikate cha kikundi cha wakina mama wajasiriamali (Kiwawanyu) kimezinduliwa katika Wilaya ya Kisarawe, Mkoani Pwani.
Balozi wa Uturuki Nchini Tanzania DR. Mehmeti amezindua kiwanda hicho cha mikate ambacho kimefanikishwa kwa ushirikiano wa Ubalozi na serikali ya Wilaya.
Ubalozi wa Uturuki umewezesha upatikanaji wa mashine za kuoka mikate na Halmashauri ilikipatia kikundi hichi mkopo wa milioni 20.
Uzinduzi wa kiwanda hicho, pia ulihudhuriwa na Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dk.Alex Malasusa.
Katika ukarasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Nickson Simon amesema “kiwanda hichi kitatoa nafasi kwa kinamama kujikimu na pia kupata ujuzi mpya – ikiwa malengo yetu nikujenga ujuzi ili kujenga uwezo wa kujitegemea katika uzalishaji.