Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Vikundi vya wajasiriamali vyakabidhiwa hundi ya bilioni 2

Vikundi vya wajasiriamali vyakabidhiwa hundi ya bilioni 2

0 comment 124 views

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla amekabidhi hundi ya Shilingi Bilioni 2 kwa vikundi 97 vya kujikwamua kiuchumi kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya asilimia 10 ya mapato ya ndani.

Mapato hayo hutengwa kwaajili ya mikopo ya kuwaendeleza wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi hundi iliyoambatana na maonyesho ya wajasiriamali katika viwanja vya Mnazi Mmoja, RC Makalla amepongeza Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kwa kutekeleza agizo la serikali la kuwezesha wananchi kiuchumi.

Aidha RC Makalla amevitaka vikundi vinavyokopeshwa kurejesha fedha hizo kwa wakati ili ziweze kusaidia vikundi vingine.

Hata hivyo RC Makalla amezielekeza Manispaa nyingine za Mkoa huo kutekeleza takwa la kisheria kwa kutoa 10% ya Mapato ya ndani kuviwezesha vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

RC Makalla pia ametoa wito kwa wananchi kununua bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali wazawa ili kuinua uchumi wa Taifa na kutoa wito kwa wajasiriamali kuwa wabunifu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Jumanne Shauri amesema katika Bilion 2 zilizotolewa, vikundi 46 vya Wanawake vimepata milion 980, vikundi 43 vya vijana Shilingi Milion 890 na vikundi 8 vya watu wenye ulemavu Milioni 157.

Maonyesho hayo yamehudhuriwa na pia na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Wabunge wa majimbo ya Ilala, Segerea na Ukonga, Mstahiki meya Ilala, Katibu tawala wa Ilala na watu mbalimbali.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter