Home KILIMOKILIMO BIASHARA Serikali kuanzisha mnada wa chai

Serikali kuanzisha mnada wa chai

0 comment 144 views

Serikali ya Tanzania imesema itaanzisha mnada wa zao la chai ili kumsaidia mkulima kupata bei inayotokana na ushindani katika soko.

Akifungua mkutano wa wadau wa sekta ya chai nchini uliofanyika mkoani Iringa, Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema mnada huo hautakuwa na tozo.

“Serikali imeamua kuanzisha mnada wa chai, hofu ni nyingi za kihistoria na tunazodhani kwamba tunaweza tusifanikiwe, jambo la kwanza litakalotufanya tushindwe ni sisi wenyewe kutokuwa tayari,” amesema Bashe na kusisitiza kuwa ni lazima mnada huo uanze mwaka huu.

Ameeleza kuwa uanzishwaji wa mnada huo ambao hatua zake zimekamilika, unakwenda sambamba na uanzishwaji wa maabara, maghala ya kuhifadhi zao hilo pamoja na ujenzi wa mazingira mazuri ya biashara ya majani ya chai.
“Mnada hautakuwa na tozo kwani serikali imekubali pia kuzibeba tozo hizo kwa manufaa ya taifa na wazalishaji wa zao hilo,” alisema bila kuzitaja tozo hizo.
Alisema kuanzishwa kwa mnada huo kutaongeza tija na ufanisi kwenye sekta ya chai utakaokuwa na manufaa na faida nyingi kwa wakulima wa zao hilo nchini.
Akitoa mfano alisema mnada huo utapunguza gharama za usafirishaji, utawezesha kutawala bei yake sokoni, kuongeza uwazi na uhakika wa ubora wa madaraja ya chai.

Taarifa iliyotolewa kwenye mkutano huo inaonesha zao hilo kwa sasa linalimwa katika wilaya 12 katika mikoa sita ya Mbeya, Kilimanjaro, Iringa, Tanga, Njombe na Kagera huku kukiwa na hekta 23,805 zilizopandwa na kati yake hekta 12,207 ni za wakulima wakubwa na hekta 11,598 za wakulima wadogo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter