Home BIASHARA Kijaji: changamkieni fursa za biashara Afrika

Kijaji: changamkieni fursa za biashara Afrika

0 comment 142 views

Wafanyabiashara nchini wameshauriwa kuhakikisha wanatumia fursa ya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi nane za majaribio za kuuza bidhaa chini ya Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) kwa kupeleka bidhaa zenye viwango na ubora wa kimataifa.
Uuzaji huo wa bidhaa unatarajiwa kuanza Julai 1, 2023.
Wito huo umetolewa na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) wakati wa mkutano wa kuwajengea uwezo na kuwahamasisha wafanyabiashara kuhusu kuchangamkia fursa za biashara chini ya AfCFTA uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Aidha, Dkt Kijaji amesema kuwa malighafi zikipelekwa nje ya nchi zinawanyima Watanzania ajira na zinapochakatwa na kuletwa nchini zinauzwa kwa gharama kubwaa.

Amesema “ni bora kutumia soko la AfCFTA ambalo masharti yamepunguzwa na unaweza kuuza bidhaa katika nchi 54 bila ushuru.
Wanawake na vijana mmefanya nini kumfanya Rais wetu kuwa kinara? Inabidi tukae tuzungumze kwa pamoja nini kinatukwamisha? Kwa nini tupeleke pamba nje badala ya nguo? Rais Samia ameamua, ni lazima tuamue kwenda kutoa huduma kimataifa.”
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Ally Gugu amesema Tanzania ni sehemu rasmi ya Mkataba wa AfCFTA ambapo nchi wanachama pamoja na sekretarieti wameanzisha nyenzo inayotengeneza mazingira rahisi kwa walioibaini fursa kuwawezesha kuuza.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI), Leodger Tenga,
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisis ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Gilead Teri na Nebart Mwapwele ambae ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) wamesema wapo tayari kuchangamkia fursa ya soko hilo linalokadiriwa kuwa na watu bilioni 1.4 lenye pato la pamoja ya thamani ya dola trilioni 1.2

Wakurugenzi hao wametakiwa wafanyabiashara watanzania kuja na mpango wa bidhaa kumi muhimu kwa ajili ya kuuza katika eneo huru la biashara Afrika ifikapo julai mosi 2023.

Aidha, Baadhi ya Wafanyabiashara Watanzania walioshiriki mkutano huo walijitokeza na kusema wako tayari kuanza kupeleka bidhaa zao ikiwemo kahawa na katani katika Soko la AfCFTA .

Wafanyabiashara walio tayari wanaweza kutuma taarifa zao kupitia barua pepe ya afcfta.gti@mit.go.tz

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter