Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIBIASHARA Watalii wafanya utalii kwa kutumia farasi

Watalii wafanya utalii kwa kutumia farasi

0 comment 273 views

Watalii zaidi ya 20 kutoka mataifa ya Australia na Marekani wametembelea Hifadhi ya Taifa Arusha na kufanya utalii wa farasi (Horse Riding).

Akizungumza kabla ya kuanza kwa zoezi hilo la kutalii kwa kutumia farasi Steven Pilcher ambaye ni Mkurugenzi kutoka kampuni ya Kaskazi Safari amesema utalii huo wa farasi hauhitaji uzoefu mkubwa.

“Faida ya kufanya utalii kwa kutumia farasi hauhitaji uzoefu mkubwa kwani kuna wakufunzi na waongoza watalii wabobevu hivyo utapata kujifunza na pia nafasi ya kuwaona kwa karibu zaidi wanyama pori, ” ameeleza Pilcher.

Ameeleza kuwa mtu anaweza kufundishwa jinsi ya kutalii na farasi na kuweza kuwaona kwa ukaribu kabisa wanyama kama twiga, tembo na kiboko.
Afisa Uhifadhi anayesimamia kitengo cha utalii katika Hifadhi ya Taifa Arusha Jerome Ndazi, amesema licha ya kuwepo utalii wa magari ambao ni maarufu zaidi, utalii wa farasi ni moja ya mazao ya utalii yanayopatikana katika Hifadhi ya Taifa Arusha.

“Hifadhi hii ina aina nyingine za mazao ya utalii ambayo mtalii anaweza kuyafurahia kama upandaji wa Mlima Meru, uendeshaji wa baiskeli, na kupiga makasia”.
Kaskazi Horse Safaris Worldwide ni moja ya watoa huduma wa utalii ambao wanafanya shughuli za utalii huu kaskazini mwa Tanzania ikiwemo katika Hifadhi bora barani Afrika – Serengeti na Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter