Home BIASHARAUWEKEZAJI TCC yapongezwa kwa uwekezaji

TCC yapongezwa kwa uwekezaji

0 comment 62 views

Kampuni ya Sigara nchini Tanzania (TCC) imepongezwa kwa utekelezaji wa malengo ya ubinafsishaji na pamoja na kuunga mkono azma ya serikali ya awamu ya tano ya serikali ya viwanda.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuitembelea kampuni hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), Suleiman Sadiq aliyeambatana na Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya ameipongeza TCC Plc kwa mafanikio makubwa waliyoyapata sambamba na kuonyesha dhamira ya kuunga mkono serikali kuelekea Tanzania ya viwanda pamoja na kutaka uongozi na wafanyakazi wa kampuni hiyo kuendelea kuchapa kazi.

“TCC Plc ni mfano mzuri unaopaswa kuigwa na wengine kwani imekuwa imara katika ulipaji wa kodi serikalini”. Amesema Sadiq.

Kwa upande wake, Waziri Manyanya amesema TCC Plc imeonyesha uwezo mkubwa kwa sababu wakati makampuni mengine yanabinafsishwa kwa nyakati sawa hayakufanikiwa kujiendeleza. Wakati huo huo, Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo amesema kampuni hiyo imekuwa ikitoa kodi serikalini na mwaka jana, wameweza kulipa kiasi cha Sh. 227 bilioni zikiwa ni kodi za ongezeko la thamani  (VAT) , mapato na ushuru wa bidhaa.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter