Home VIWANDA Majaliwa atoa pongezi kwa kiwanda cha Morris Philip

Majaliwa atoa pongezi kwa kiwanda cha Morris Philip

0 comment 80 views
Na Mwandishi wetu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepongeza ujenzi wa Kiwanda cha Morris Philip Tanzania Limited mkoani Morogoro na kuwataka waajiriwa katika kiwanda hicho kufanya kazi kwa bidii na uadilifu ili kuvutia wawekezaji zaidi kuja kuwekeza hapa nchini.

Majaliwa ametoa pongezi zake kwa muwekezaji wa kiwanda hicho kwa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais Magufuli katika kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda akiongeza kuwa serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuwatoa wananchi wake katika umaskini.

Mbali na hayo, Waziri Mkuu pia amesema anazo taarifa kuwa kampuni ya Morris Philip ndiyo inaongoza kwa kununua tumbaku inayolimwa hapa nchini hivyo kitendo cha kampuni hiyo kuwekeza kwa kuanzisha kiwanda ni ishara kuwa ununuzi wa tumbaku pia utaongezeka.

Kwa upande wake, Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage amewataka wakazi mkoani Morogoro kutumia fursa ya kuanzishwa kwa kiwanda hicho mkoani humo kujipatia ajira na kujiingizia kipato.

Naye mwakilishi wa kiwanda hicho hapa nchini Can Uslu amedai kuwa kampuni hiyo iliridhishwa na utulivu uliopo hivyo kuamua kuja kuwekeza hapa nchini. Ameongeza kuwa kiwanda hicho kinatarajia kutoa ajira rasmi takribani 100 na zile zisizo rasmi zaidi ya 2000  na kusisitiza kuwa bidhaa zitakazozalishwa zitakuwa na ubora wa kimataifa.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter