Home KILIMOKILIMO UFUNDI Uzalishaji muhogo ni tani 8.6 badala ya tani 30 kwa hekta

Uzalishaji muhogo ni tani 8.6 badala ya tani 30 kwa hekta

0 comment 217 views

Imeelezwa kuwa uzalishaji wa muhogo nchini ni tani 8.6 badala ya tani 30 kwa hekta ambacho ndicho kiwango cha uzalishaji wenye tija.

Uzalishaji mdogo katika mazao ya muhogo na viazi vitamu umekuwa ni kichocheo kwa watafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kutumia teknolojia zitakazowezesha kuharakisha uzalishaji wa mbegu bora zinazostahimili mashambulizi ya virusi vinavyotajwa kupunguza tija katika uzalishaji wa mazao hayo.

Hayo yamebainishwa Novemba 04, 2024 katika ufunguzi wa mafunzo kwa watafiti wa viazi na muhogo ya siku nne Mkoani Mwanza katika kituo cha TARI Ukiriguru.

Mafunzo hayo ambayo ni matokeo ya ushirikiano wa TARI na Taasisi zingine zikiwemo Taasisi ya Kimataifa ya Kilimo cha kitropiki (IITA), CIAT na Maabara ya uchunguzi wa virusi ya Ujerumani (DSMZ) unaolenga kujengeana uwezo wa teknolojia za uzalishaji wa haraka wa mbegu za mazao ya mizizi zisizokuwa na magonjwa ili kuwafikia wakulima kwa wakati na hivyo kuchangia kuongezeka tija.

Mtafiti wa mihongo kituo cha TARI Ukiriguru Salum Kasele amesema wastani wa muda wa kuanza kutafiti mbegu hadi kuisajili kwa kutumia njia ya kawaida inaenda hadi miaka kumi na kwamba kupitia mafunzo hayo muda wa kuzalisha mbegu hadi kumfikia mkulima unategemewa kufikia wastani wa miaka mitano.

Kwa upande wa viazi vitamu, Mkuu wa programu ya Utafiti wa zao hilo kituo cha TARI Ukiriguru, Dkt Hadija Ally anasema kwa takwimu za mwaka 2022/2023 uhitaji wa mbegu bora za viazi vitamu kwa kanda ya ziwa ilikuwa vipando milioni 23 huku idadi iliyotumiwa na wakulima ilikuwa ni vipando chini ya milioni 5 tu.

Kuhusu athari za ugonjwa wa virusi vya viazi vitamu, Dkt Hadija amesema mkulima hawezi kupata mavuno ya aina yoyote endapo shamba lake limeathiriwa kwa asilima 100 na virusi. Hivyo ujio wa teknolojia ya kutambua na kuzalisha mbegu stahimilivu dhidi ya virusi utaleta tija katika kilimo cha viazi vitamu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter