Home KILIMOKILIMO BIASHARA Mradi wa 27.8bn kusaidia wakulima, wajasiriamali wazinduliwa

Mradi wa 27.8bn kusaidia wakulima, wajasiriamali wazinduliwa

0 comment 329 views

Mradi wenye thamani ya Euro Million 9.5 sawa na Tsh. 27.8 Billion wa Growing Together unaolenga kusaidia wajasiriamali wadogo na wakati umezinduliwa.

Mradi huo ambao unafadhiliwa na Serikali ya Kifalme ya Norway kupitia Shirika la Maendeleo la Norway (Norad) na Dkt. Suleiman Serera, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo (Ushirika na Umwagiliaji) Novemba 06, 2024 katika Hoteli ya Four Points by Sheraton, jijini Dar es Salaam.

Mradi huo wa miaka mitano, umelenga kusaidia wajasiriamali wadogo na wa kati (SMEs 10), wakulima wadogo 60,000 na wanunuzi wakubwa (Off Takers) 2 kwa mazao ya mchele, mahindi, maharage na alizeti katika Mikoa ya Dodoma, Iringa, Mbeya na Morogoro kwa kutatua changamoto ya tija ndogo, upatikanaji wa mikopo nafuu kwa wasindikaji na wakulima, mabadiliko ya tabianchi, ajira kwa vijana na wanawake.

Dkt. Serere amesema mradi huo umelenga kuongeza tija, kuimarisha upatikanaji wa mikopo yenye riba nafuu, kuimarisha ushirika wa vijana na wanawake na utasaidia wasindikaji na wakulima kulifikia soko la ndani na nje ya nchi na utachangia kufikia malengo ya Ajenda 10/30.

“Mradi huo ni mafanikio yaliyotokana na Hati ya Makubaliano (MoU) iliyosainiwa kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Kilimo na Serikali ya Kifalme ya Norway kupitia Wizara ya Mambo na Maendeleo ya Kimataifa ya Norway kufuatia ziara ya kikazi ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Norway tarehe 12-14 Februari 2024, ambapo Rais alisisitiza utekelezaji wake uwaguse wakulima na wasindikaji nchini,” ameeleza Serere.

Mradi huo unaendana na maeneo ya ushirikiano ambayo yapo kwenye MoU iliyosainiwa ikiwemo uwezeshaji wa Sekta Binafsi kuwekeza katika Sekta ya Kilimo kwa kupata mikopo yenye riba nafuu na kuimarisha ushirika wa vijana na wanawake katika Mifumo ya Uzalishaji wa Chakula nchini.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter