Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIFEDHA Jumuiya ya Wahasibu Wakuu Afrika yatakiwa kuweka mifumo usimamizi fedha za umma

Jumuiya ya Wahasibu Wakuu Afrika yatakiwa kuweka mifumo usimamizi fedha za umma

0 comment 37 views

Jumuiya ya Wahasibu Wakuu wa nchi za Afrika wametakiwa kuandaa mapendekezo yanayohusu umuhimu wa mifumo madhubuti ya usimamizi wa fedha za umma inayoweza kukabiliana na changamoto zinazojitokeza duniani.

Changamoto hizo ni pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchi, mabadiliko ya kiteknolojia na mabadiliko ya kiuchumi.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa Disemba 02, 2024 wakati akifungua Mkutano wa Pili wa Mwaka wa Jumuiya ya Wahasibu Wakuu wa nchi za Afrika (AAAG) unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha ambao umebeba kauli mbiu isemayo “Kujenga Imani ya Umma katika Mifumo ya Usimamizi wa Fedha za Umma kwa Ukuaji Endelevu”.

Bashungwa amesisitiza kuwa uwepo wa matumizi ya mifumo thabiti itapunguza gharama za usimamizi, kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato na kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wananchi wengi zaidi.

Aidha, Bashungwa ametoa wito kwa Jumuiya hiyo kupendekeza mbinu mpya za kuboresha usimamizi wa fedha za umma kupitia matumizi ya teknolojia ya kidijitali ili kuongeza ufanisi, uwazi na uwajibikaji.

Bashungwa ameitaka Jumuiya hiyo kuona namna ya kukuza ushirikiano wa karibu kati ya Serikali, Sekta Binafsi na Asasi za kiraia, katika usimamizi wa fedha za umma hasa katika kutekeleza miradi ya maendeleo.

Kwa upande wake, Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba ameeleza usimamizi madhubuti wa fedha unasaidia wananchi kujenga tabia ya kulipa kodi kwa hiari ambapo Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zinazofanya vizuri.

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba.

Nchemba amethibitisha hayo kwa kutolea mifano ya miradi iliyokamilika na inayotekelezwa nchini ikiwemo Bwawa la Kufua Umeme, miradi ya umwagiliaji, miundombinu ya barabara, ujenzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo – Busisi) pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa (SGR)

Naye, Mhasibu Mkuu wa Serikali wa Ufalme wa Lesotho na Mwenyekiti wa Jumuiya ya AAAG, Malehlonolo Mahase ameeleza kuwa kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo kuna malengo na manufaa muhimu katika usimamizi bora wa fedha za umma na kuimarisha utendaji katika nchi za Afrika.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter