Home BIASHARA Mnada wa madini ya vito warejeshwa, kufanyika Desemba 14

Mnada wa madini ya vito warejeshwa, kufanyika Desemba 14

0 comments 292 views

Mnada wa madini ya vito ambao ulisimama kwa muda umepangwa kufanyika tena Desemba 14, 2024.

Waziri wa Madini Anthony Mavunde anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mnada huo unaotarajiwa kufanyika katika mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara, ili kuyaongezea thamani madini hayo.

Akizungumza Desemba 12, 2024, Mavunde amesema madini ya vito, yanafanyiwa mnada kama mkakati wa kuyatangaza na kuyaongezea thamani kimataifa.

Waziri Mavunde amesema utaratibu wa kufanya mnada huo ni jitihada za Serikali za kudhibiti utoroshwaji wa madini hayo nje ya nchi na pia kuwasaidia wachimbaji kuuza madini yao kwa bei ya ushindani inayoendana na soko la dunia.

Amesema, mnada huo utashirikisha wanunuzi kutoka ndani na nje ya nchi na atakayenunua madini hayo katika mnada ni atakayeshinda bei iliyowekwa.

“Mnada huu utaendeshwa kwa usalama mkubwa kwa kuwa madini hayo hususan Tanzanite yana thamani kubwa. Serikali imeimarisha ulinzi ili kujihadhari na watu wasio waaminifu,”amesema Waziri Mavunde.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!