Home BENKI Mikopo ya hadi Milioni 150 kutolewa ndani ya masaa 24

Mikopo ya hadi Milioni 150 kutolewa ndani ya masaa 24

0 comment 101 views

Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NMB Ineke Bussemaker amewaambia waandishi wa habari kuwa benki hiyo imeanza kutoa mikopo ya hadi Sh. 150 milioni kwa wafanyakazi nchini ndani ya siku moja huku muda wa marejesho wa mikopo hiyo ukiongezeka na kufikia miaka sita. Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa mikopo hiyo itajumuisha wafanyakazi kutoka sekta binafsi na serikalini bila ubaguzi wowote na kwamba, kinachoangaliwa ni mikataba ya kudumu au ile ya muda mrefu.

Imeelezwa kuwa mfanyakazi anaweza kupatiwa mkopo wa hadi Sh.150 milioni ambao unaweza kulipwa kidogo kidogo kwa kipindi cha miaka sita. Vilevile, NMB imepunguza riba kwa wafanyakazi wote  kutoka asilimia 19 mpaka 17.

Utoaji wa mikopo hiyo ni muendelezo wa sekta ya benki hapa nchini kutoa mikopo ya kima kilichoongezeka na masharti nafuu, huku riba za benki zikipungua kwa viwango tofauti tofauti.

Akiwa mjini Dodoma mwishoni mwaka jana, Rais Magufuli aliagiza benki kuangalia uwezekano wa kupunguza riba ya mkopo na baadhi ya benki kama CRDB, BOAT na NMB zimeonyesha kumuunga mkono na kufanya hivyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter