• Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
Sunday, June 26, 2022
  • Login
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
No Result
View All Result

Mfumo mpya wa visa na vibali vya ukaazi vya kielektroniki kukuza diplomasia ya uchumi

Mfumo huu mpya unatarajia kufikia malengo ya eerikali ya kukuza diplomasia ya uchumi, kuchochea kasi ya maendeleo na uchumi wa viwanda.

Patricia Richard by Patricia Richard
November 27, 2018
in UWEKEZAJI
0
Share on FacebookShare on Twitter

Na. Immaculate Makilika – MAELEZO

Serikali imesema mfumo mpya wa visa na vibali vya ukaazi vya kielektroniki unatajwa kuwa na faida lukuki kwa nchi ikiwemo kukuza sera ya diplomasia ya uchumi, sera ya viwanda, kusaidia ongezeko la watalii wanaokuja nchini pamoja na kuongeza ukusanyaji wa madurufu ya Serikali.

Akizungumza jana, jijini Dar es salaam, wakati akizindua mfumo wa visa na vibali vya ukaazi vya kielektroniki, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, alisema kuwa mfumo huu mpya unatarajia kufikia malengo ya Serikali ya kukuza diplomasia ya uchumi, kuchochea kasi ya maendeleo na uchumi wa viwanda, sambamba na hilo raia wa kigeni wanaweza kuomba huduma hiyo wakati wowote na mahali popote duniani.

“Ni imani yangu kuwa mfumo huu mpya utatatua changamoto zote zilizokuwepo awali, lakini pia utarahisisha upatikanaji wa huduma kwa raia wa kigeni. Ni muhimu kwa mfumo huu kuunganishwa na mifumo mingine ya Idara ya Kazi, Kituo cha Uwekezaji, Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), pamoja na Mfumo wa Malipo wa Kieletroniki Serikalini (GePG), ambayo itamsaidia mteja kupata huduma kwa urahisi bila usumbufu wowote” alisema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu Majaliwa, aliongeza kuwa mfumo huo utasaidia kutoa huduma kama ambavyo Serikali imekusudia, sambamba na kusaidia nchi katika masuala ya ulinzi na usalama.

Aidha, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga alisema kuwa mfumo huo utasaidia kukuza sekta ya utalii, ambapo kwa mwaka watalii milioni moja hadi mbili pekee wanafika  nchini, ambapo fedha za kigeni zinapatikana katika sekta hiyo ya utalii.

“Matarajio yangu kwamba mfumo huu mpya  wa  visa na vibali vya ukaazi  vya kielektroniki, utasaidia kuboresha na kuvutia wawekezaji,  sambamba na kuleta watalii nchini”

Pia, Waziri Mahiga alisema Wizara yake itaelimisha Jumuiya ya Mabalozi kuhusu huduma hiyo, ikiwa ni sambamba na kufanya diplomasia ya uchumi.

Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa Uhamiaji nchini, Dkt. Anna Makakala alisema kuwa mfumo huo mpya wa visa na vibali vya ukaazi  vya kielektroniki utasaidia kuimarisha usalama, uwekaji wa kumbukumbu, pamoja na kuwezesha Idara ya uhamiaji kupata taarifa na kuzifanyia kazi kabla ya mgeni kuwasili nchini, pamoja na kukusanya madurufu ya serikali bila upotevu

“Kuanzia Januari 31, mwaka 2018  hadi Novemba 25, 2018 jumla ya hati mpya za kusafiria za kielektroniki 55, 177 zimetolewa, ambapo zaidi ya shilingi bilioni 7 zimepatikana kutokana na malipo ya hati mpya za kusafiria za kielektroniki” alisema Kamishna Mkuu wa Uhamiaji

ADVERTISEMENT

Aidha, ifikapo Januari 2019 huduma ya upatikanaji wa hati mpya za kusafiria za kielektroniki itapatikana katika balozi zote za Tanzania ili kuwarahisishia huduma watanzania au raia wa kigeni walioko nje ya nchi.

Mradi wa Uhamiaji Mtandao unaohusisha mfumo wa hati ya kusafiria ya kielektroniki, mfumo wa visa na vibali vya ukaazi vya kielektroniki ambayo ni awamu ya pili, pamoja na mfumo wa kuzuia na kudhibiti wahamiaji haramu wanaoingia nchini.

Tags: Augustine MahigaBRELAKassim MajaliwauchumiUhamiajiviwanda
Patricia Richard

Patricia Richard

Next Post
Ujenzi SGR washika kasi

Ujenzi wa SGR kutumia mataruma yanayozalishwa nchini

Discussion about this post

Habari Mpya

Miamala ya simu yaongeza Pato la Taifa

June 24, 2022

Mapendekezo bima ya afya kwa wote

June 23, 2022

Kilimo biashara, sekta yenye fursa za uwekezaji

June 23, 2022

Turkish Airlines yarejesha safari zake KIA

June 22, 2022
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla akizungumza katika warsha ya viongozi wa Serikali wa mkoa na Bank ya NMB.

Benki ya NMB yapongezwa

June 22, 2022

Rais Samia azindua taasisi Zanzibar

June 20, 2022

KUHUSU SISI

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905. PesaTu inamlenga kila mtu ambaye kwa namna moja au nyingine anaguswa na anapenda kujua/ kufuatilia masuala mbalimbali ya kiuchumi ya nchi ikiwemo ujasiriamali, uwekezaji, viwanda, kilimo na hisa.

LATEST

Miamala ya simu yaongeza Pato la Taifa

by Pesatu Reporter
June 24, 2022
0

Miamala ya fedha kwa njia ya simu imechangia kuongezeka kwa pato la Taifa kutoka asilimia 40 mwaka 2013 hadi kufikia...

Mapendekezo bima ya afya kwa wote

by Pesatu Reporter
June 23, 2022
0

Mapendekezo yamepitishwa kwa kila Mtanzania kuwa na bima ya afya. Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM (NEC) leo 23...

RECOMMENDED

Waziri Mwijange aja na orodha ya viwanda visivyofanya kazi

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

  Na Mwandishi wetu. Baada ya Rais John Magufuli kuonyesha kukerwa na kitendo cha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji...

Nane Nane itumike kama darasa huru kwa wakulima

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

Na Mwandishi wetu Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imejitolea kuwapa mafunzo ya siku moja wakulima mkoani Lindi...

No Result
View All Result
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI

© 2022 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In