Wafanyabiashara mkoani Tanga wamehamasishwa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ili kuwa na uhakika wa matibabu na kuepuka kutumia fedha nyingi pindi wanapougua. Wito huo umetolewa na Afisa Matekelezo wa NHIF mkoani humo Sophia Kaku alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya sita ya biashara ya kimataifa yanayoendelea mkoani humo katika viwanja vya Mwahako. Afisa huyo ametoa wito kwa wafanyabiashara kujiunga na huduma ya bima kwani inasaidia kuokoa fedha nyingi ambazo hutumika pindi mtu anapoumwa ghafla huku akisisitiza kuwa kupitia mpango wa bima ya afya, huduma mbalimbali zinapatikana bila mgonjwa kutumia gharama ya ziada.
Wadau ufugaji nyuki watakiwa kuchangamkia fursa
Tanzania ni nchi ya pili kwa uzalishaji wa asali barani Afrika na inashika nafasi ya 14 dunia. Ethiopia, ndio nchi...
Discussion about this post