Home VIWANDA Wachina kujenga kiwanda cha dawa

Wachina kujenga kiwanda cha dawa

0 comment 107 views

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ametangaza kuwa, mwekezaji kutoka China anatarajia kujenga kiwanda cha dawa kilicho na thamani ya Sh. 45 bilioni hapa nchini. Hayo yamebainishwa katika kikao kilichohudhuriwa na wawekezaji hao wanaofahamika kama Fosunpharma, Waziri Ummy Mwalimu, Waziri wa Viwanda na Uwekezaji Charles Mwijage pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Geoffrey Mwambe.

Waziri Ummy amebainisha kuwa mara baada ya ujenzi wa kiwanda hicho kukamilika, huduma zitakazotolewa zitasaidia kupunguza idadi ya vifo vya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano hapa nchini kutokana na uzalishaji wa sindano ya Artesun inayosaidia kupambana na Malaria kali.

Naye Waziri wa Viwanda na Uwekezaji Charles Mwijage ameeleza kuwa viwanda vya kuzalisha mafuta ya kula na dawa ni baadhi ya maeneo ambayo bado hayajafanikiwa. Vilevile, Mwijage ametoa pongezi kwa Balozi wa Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki kwa kufanikisha kampuni ya Fosunpharma kufika hapa nchini.

Kwa upande wake, Dk. Ashok Pandey, Mkurugenzi Mtendaji wa Gullin Pharmaceuticals Tanzania ambayo ni kampuni tanzu ya Fosunpharma amesema hivi sasa wapo katika mchakato wa kutafuta eneo la kujenga kiwanda hicho.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter