Home BENKI Riba KCB yaendelea kushuka

Riba KCB yaendelea kushuka

0 comment 114 views

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB Tanzania Cosmas Kimario amesema benki hiyo bado itaendelea kupunguza riba ya mikopo ili kuwanufaisha wananchi wengi zaidi. Kimario amesema hayo katika uzinduzi wa tawi jipya la benki hiyo eneo la Mbagala Zakhem jijini Dar es salaam.

 

Kimario amedai kuwa, wao kama taasisi ya fedha wanafanya hivyo kufuatia ombi la Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji la kuwahimiza washushe riba zao. Hivi sasa, benki hiyo imepunguza riba kutoka asilimia 20 ya hapo awali hadi asilimia 15 huku wakiendelea kuangalia uwezekano wa kuishusha zaidi kulingana na kiwango anachochukua mkopaji.

 

Mbali na kupunguza riba, KCB Tanzania pia inajipanga kusogeza huduma zake karibu zaidi na wateja katika maeneo mbalimbali ili kuondoa kero ya kutumia muda mrefu kusaka huduma.

 

Naye, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji ametoa wito kwa benki hiyo kuangalia namna ya kuwafikia wale wasio kwenye sekta rasmi hasa kilimo ili kusaidia kuongeza uzalishaji wa malighafi zitakazokidhi mahitaji ya viwanda.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter