Home BIASHARAUWEKEZAJI Uboreshaji wa miundombinu wavutia wawekezaji

Uboreshaji wa miundombinu wavutia wawekezaji

0 comment 43 views

Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Kuendeleza Kilimo Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Geoffrey Kirenga amesema uwekezaji mkubwa unaoendelea kufanywa na serikali katika kuboresha miundombinu ya barabara na umeme vijijini umechochea uzalishaji katika sekta ya kilimo na kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda.

 

Kirenga amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa, wawekezaji katika sekta ya kilimo wameendelea kuvutiwa na maboresho mbalimbali yanayoendelea katika sekta ya miundombinu.

 

Mbali na hayo, Mkurugenzi huyo pia alipata fursa ya kuzungumzia kuhusu Awamu ya Pili ya Mpango wa Maendeleo ya Kilimo (ASDP II) na kusema kuwa, mpango huo utaleta mageuzi ya aina yake katika sekta za kilimo na viwanda, na hivyo kuinua maisha ya wananchi wengi.

 

Kirenga pia ameeleza kuhusu kazi kubwa inayofanywa na kituo hicho katika kuwaunganisha wakulima wa ubia kati ya serikali na sekta binafsi na wataalamu wa kilimo na masoko ili kuwainua wakulima katika ukanda huo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter