Home BIASHARA TRA yataifisha bodaboda 52

TRA yataifisha bodaboda 52

0 comment 123 views

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere ametangaza kutaifishwa kwa pikipiki 52 ambazo zilikamatwa zikisafirisha bidhaa kimagendo kutoka nchini Kenya kuelekea mkoa wa Kilimanjaro. Kichere amesema hayo wakati akikabidhi pikipiki hizo kwa jeshi la polisi la Kilimanjaro ili zitumike kusaidia mapambano dhidi ya biashara ya magendo.

“Sisi tukikamata tunataifisha na kuwa mali ya serikali,pikipiki hizi ni sehemu tu kwa sababu tumekamata vitu vingi katika maeneo haya ya kaskazini, tumekamata magari, tumekamata mizigo ya magendo. Kwa mfano, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2017/2018 kulikamatwa bidhaa za magendo zenye thamani ya Sh. 2.9 bilioni na kodi iliyokusanywa kwenye bidhaa hizo zilizolipishwa kodi na faini kwa mwaka huo wa fedha ni Sh. 758 milioni”. Amesema Kamishna huyo.

Naye Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro Hamisi Issa amesema usafiri huo utagawanywa kwa wilaya zilizoathirika zaidi na biashara za magendo na kutoa ahadi kwa Kamishna Kichere kuwa zitatumika kufanya kazi iliyokusudiwa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter