Home KILIMO Kampeni ya kutibu mikorosho yazinduliwa

Kampeni ya kutibu mikorosho yazinduliwa

0 comment 116 views

Meneja wa Bodi ya korosho tawi la Tanga, Ugumba Kilasa amezindua rasmi kampeni ya kutibu miti ya mikorosho katika wilaya tatu mkoani humo kwa lengo la kupambana na changamoto ya wadudu kushambulia zao hilo. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo katika kijiji cha Bawa wilayani Mkinga, Kilasa amesema kampeni hiyo itafahamika kama “tibu mikorosho ongeza kipato” na itafanyika katika wilaya za Muheza, Mkinga pamoja na Pangani.

 

Meneja huyo ametoa wito kwa wakulima na wadau wa sekta hiyo kwa ujumla kuitumia vizuri kampeni hiyo na kunyunyizia dawa kwa wakati unaotakiwa ili kukabiliana na milipuko ya magonjwa ya mnyauko wa majani na maua ya zao hilo. Hadi kufikia sasa, Kilasa ameeleza kuwa lita 20,000 za dawa ya maji pamoja na tani 60 za dawa ya safa ya unga tayari zimepokelewa ili kutekeleza kampeni hiyo.

 

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama kikuu cha wakulima wa korosho mkoa wa Tanga, Mashi Sopa amesema chama hicho kimejipanga kupambana na changamoto ya walanguzi wa korosho na kuwatoa hofu wakulima kuhusu usalama wa mazao yao.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter