Home KILIMO TADB,NIRC kuboresha miundombinu ya umwagiliaji

TADB,NIRC kuboresha miundombinu ya umwagiliaji

0 comment 181 views

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) pamoja na Tume ya Taifa  ya Umwagiliaji (NIRC) wameingia mkataba wa kuboresha vyanzo na miundombinu ya umwagiliaji nchini. Akiwa katika utiaji saini wa makubaliano hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB Japhet Justine amesema lengo kubwa la makubaliano hayo ni kuiwezesha NIRC kuendeleza vyanzo mbalimbali vya maji ili kuwasaidia wakulima na katika kufanya hivyo kuboresha sekta ya kilimo kwa ujumla.

Justine ameeleza kuwa hadi sasa, TADB imefanikiwa kuwezesha miradi tisa ya umwagiliaji huku mingine mine ikiwa katika hatua ya uchambuzi kabla ya kupata ufadhili. Kaimu huyo amesisitiza kuwa miradi ya umwagiliaji ina mchango mkubwa katika sekta ya kilimo kwani ni fursa mojawapo kwa wakulima kupiga hatua na kuongeza uzalishaji wa mazao pamoja na thamani ya kilimo.

“Maji yakiwapo ya kutosha yatamsaidia mkulima kuendesha shughuli zake za kilimo na kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali. Kama ilivyo kwa binadamu na mimea nayo hivyo hivyo”. Amesema Justine.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NIRC Dk. Eliakim Chitutu mbali na kuishukuru benki hiyo pia ameeleza kuwa tume hiyo imejipanga kuimarisha miundombinu ya umwagiliaji na kuikamilisha ndani ya miaka 17. Mkurugenzi huyo pia ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa sekta binafsi kuwekeza katika umwagiliaji ili kusaidia wakulima kufanya shughuli zao kwa tija zaidi na hivyo kuinua kilimo nchini.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter