Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Wajasiriamali waongezewa muda maonyesho ya chakula

Wajasiriamali waongezewa muda maonyesho ya chakula

0 comment 108 views

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi ameongeza muda wa siku mbili kuendelea maonyesho ya siku ya chakula kwa lengo la kutoa fursa kwa wajasiriamali kujifunza mbinu mbalimbali za uzalishaji huku akisisitiza umuhimu mkubwa wa maonyesho hayo katika kuchangia maendeleo ya kazi za wajasiriamali. Akizungumza katika hafla ya kufunga maonyesho hayo wilayani Wete, Balozi Seif amesema kuwa kuongeza siku za maonyesho hayo kutaongeza wigo kwa wananchi kujifunza taaluma za uzalishaji bidhaa bora.

“Maonyesho haya yataendelea hadi jumamosi hivyo ni vyema wananchi kuitumia fursa hii kutembelea maonyesho haya ili wapate mbinu mpya ya uzalishaji”. Amesema Makamu huyo wa Rais.

Pamoja na hayo, Balozi Seif pia ameagiza Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kuweka nguvu kubwa na kuimarisha kitengo cha kutafiti mazao ili kitumike kuelimisha wananchi na kitimiza azma ya serikali ya kukabiliana na tatizo la njaa.

Kwa upande wake, Naibu Waziri kutoka Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Dk Makame Ali Ussi amesema maonyesho yamefungua milango kwa wajasiriamali kwani mbali na kuwaelimisha, yamewahamisisha kupata mbinu mpya ambazo zitawasaidia kuongeza uzalishaji.

“Hii ni fursa ambayo imewawezesha wajasiriamali kupata mbinu mpya za kuzalisha hivyo ni imani yangu kwamba elimu iliyotolewa kwa wajasiriamali itaongeza uzalishaji”. Amesema Dk. Ussi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter