Home VIWANDAUZALISHAJI TADB kuhamasisha uzalishaji maziwa

TADB kuhamasisha uzalishaji maziwa

0 comment 106 views

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB), Japhet Justine amesema benki hiyo imejipanga kuhakikisha uzalishaji wa maziwa unaongezeka hapa nchini ili kutoa fursa kwa wazalishaji wadogo kuchangia ukuaji wa sekta hiyo. Justine amesema hayo wakati akizungumza na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) Prof. Philemon Wambura na kuongeza kuwa, shughuli za usindikaji wa maziwa zipo chini ya kiwango kutokana na uzalishaji duni wa maziwa, hali ambayo amedai inarudisha nyuma ukuaji.

“Fursa za kimasoko na uendelezaji wa tasnia ya maziwa ni kubwa hivyo tumejipanga kuhakikisha tunachagiza tasnia hii ili kuongeza uzalishaji na kuwaongezea kipato wazalishaji hasa wale wadogo wadogo”. Amesema Justine.

Katika maelezo yake, Kaimu huyo amesema kuwa katika kuhakikisha tasnia ya maziwa inawanufaisha wazalishaji wadogo, benki hiyo inapanga mikakati ya kuanzisha Jukwaa la Ushirikiano wa Tasnia ya Maziwa kwa lengo la kuwakutanisha wadau wa sekta hiyo ili kujadili kwa kina mipango ya kuongeza uzalishaji wa maziwa nchini.

Naye Prof. Philemon Wambura amesema NARCO imejipanga kuwawezesha wazalishaji wadogo kote nchini kwa kuwapatia huduma za ugani ili nao wapate nafasi ya kuongeza uzalishaji wa maziwa. Meneja huyo ameongeza kuwa harakati za TADB katika kuipeleka mbele tasnia ya maziwa ni jambo la kuigwa kwani zinachangia shughuli za uzalishaji.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter