Home VIWANDAMIUNDOMBINU Serikali yamwaga bilioni 21 Mtwara

Serikali yamwaga bilioni 21 Mtwara

0 comment 116 views

Serikali kupitia mradi wake wa uendelezaji miji mkakati (Tanzania Strategic Cities Project) imetenga Sh. 21.7 bilioni kwa ajili ya kujenga miundombinu mbalimbali ya maendeleo katika Manispaa ya Mtwara Mikindani ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara nne za mitaa kwa kiwango cha lami, ujenzi wa maeneo matatu ya kupumzikia (Recreation Center), mfereji mkubwa wa kuondoa maji ya mvua, ujenzi wa soko la kisasa na vilevile kituo cha daladala katika eneo la Mikindani.

Akizungumza wakati wa kukagua miradi hiyo,  Mkuu wa wilaya ya Mtwara Evod Mmanda amesema fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo zimetolewa kwa mkopo na Benki ya dunia (WB) na kwamba ujenzi wa miradi hiyo yote unatarajiwa kukamilika hadi kufikia mwezi Oktoba 2019.

Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa amesema mji wa Mtwara utabadilika na kuwa na muonekano mzuri baada ya miradi hiyo kukamilika huku akidai kuwa,ni hatua nzuri kuitayarisha manispaa kuwa na sifa ya kuwa jiji. Byanakwa pia ametoa wito kwa vijana waliobahatika kuajiriwa katika miradi hiyo kuwa waaminifu.

“Naamini baada ya kukamilika miradi hii itakuwa sehemu nyingine na pengine inaweza kupata sifa ya kuelekea kuwa jiji”. Ameeleza Mkuu huyo wa mkoa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter