Home BIASHARAUWEKEZAJI Waziri Kalemani: Maeneo yatengwe na kuboreshwa kwa uwekezaji wa viwanda

Waziri Kalemani: Maeneo yatengwe na kuboreshwa kwa uwekezaji wa viwanda

0 comment 47 views

Na Grace Semfuko-MAELEZO

WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani, ameuagiza uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Pwani kuainisha maeneo yote kwa uwekezaji wa viwanda ili kuharakisha miundombinu ya nishati ya umeme utakaosaidia kuhamasisha wawekezaji na hivyo kusaidia kukuza uwekezaji wa viwanda.

Dkt. Kalemani ameyasema hayo alipotembelea maonesho ya bidhaa za viwandani katika Viwanja vya Sabasaba vilivyopo Picha ya Ndege, Wilaya ya Kibaha Mkoani  Pwani, akasisitiza kuwa wakati Serikali ya awamu ya tano inaweka mikakati ya kuhakikisha kunakuwa na viwanda vya kutosha kuinua uchumi wa taifa watendaji wa sAerikali hiyo hawana budi kuimarisha miundombinu yake na kupanua fursa..

“Mkoa wenu huu wa Pwani ni Mkubwa na wenye ardhi na rasilimali za kutosha kabisa, ainisheni maeneo ya uwekezaji na mtuambie tuje kuweka miundombinu ya nishati, sisi tutafanya kazi hiyo haraka, kwani tunataka uwekezaji uwe mkubwa ili Nchi yetu iweze kupata manufaa makubwa kiuchumi” alisema Dkt. Kalemani.

Pia Waziri Dkt Kalemani amewataka wawekezaji nchini kuongeza bidii katika kujenga viwanda vya uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ili kuwawezesha Watanzania kupata ajira pamoja na kuiingizia Serikali pato kutokana na kodi mbalimbali za uuzwaji wa bidhaa hizo.

Waziri huyo pia ametoa wito kwa viongozi wa mikoa mbalimbali nchini kutenga maeneo ya uwekezaji ili kuwawezesha wawekezaji kutoka katika mataifa mengine kuja kuwekeza bila kuwa na vikwazo vya kiuchumi.

Pia Waziri Kalemani  amesema katika kukabilina na changamoto za miundombinu ya nguzo za miti kwa ajili ya umeme kuharibika hususani katika maeneo yenye maji mengi amewataka wadau wanaotengeneza nguzo za umeme za zege kuboresha bidhaa hiyo ili ziweze kuingia katika ushindani na hatumaye ziweze  kupata masoko zaidi.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amesema mkoa wake unafanya kila jituhada za kuhakikisha miundombinu rahizi inafikika kwenye maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya viwanda na kuwaagiza watendaji katika Halmashauri zote kutenga maeneo ya uwekezaji.

“ Sisi Mkoa wa Pwani tunayo maeneo ya kutosha kabisa katika uwekezaji, na tunafanya kila jitihada za kuhakikisha miundombinu rahisi ikiwepo ya Barabara,Maji na Umeme inafikika ili viwanda vijengwe na vianze uzalishaji wa bidhaa mara moja” alisema Mhandisi Ndikilo.

Nae Meneja  wa kiwanda kinachotengeenza nguzo za umeme za zege cha  East Africa Infrastructure Engineering Limited, Johns Peter Majura amesema wameanza kuzalisha nguzo za umeme ili kuimarisha miundombinu ya umeme kwenye maeneo mbalimbali nchini.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Asumpta Mshama amesema Wilaya yake tayari imeanza kuvutia wawekezaji kwa kutenga maeneo ya uwekezaji ambayo tayari yameanza kupata wawekezaji kutoka katika mataifa mbalimbali duniani.

Maonesho ya bidhaa za viwandani katika Mkoa wa Pwani yalifunguliwa tare 29  ili kutangaza bidhaa mbalimbali za uwekezaji katika mkoa huo na yatafungwa Nov. 3, mwaka huu

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter