Home BENKI BoT Yazibana taasisi za fedha

BoT Yazibana taasisi za fedha

0 comment 141 views

Benki kuu ya Tanzania (Bot) imezitaka taasisi ndogondogo za fedha nchini kuwasilisha  nyaraka muhimu wanazotumia kufanyia biashara hizo kuanzia wiki ijayo.

Katika taarifa iliyotolewa na Bot Desemba mwaka jana iliwataka wafanyabiashara wa biashara za kifedha ndogondogo kuwasilisha taarifa muhimu za biashara zao hususani kuhusu uendeshaji na umiliki wa taasisi hizo kabla ya January 11.

Miongoni mwa nyaraka muhimu zinazohitajika na Bot ni pamoja na leseni za biashara iliyotolewa na wakala wa usajili wa biashara (Brela),cheti cha utambuzi wa umiliki wa biashara,anuani ya mahali biashara ilipo pamoja na mawasiliano husika,ukaguzi wa hesabu wa kila mwaka,safu ya wamiliki na uongozi wa biashara husika ikiwemo bodi ya wakurugenzi,mtendaji mkuu na uraia wao pamoja na mifumo ya kiteknolojia na mawasiliano,madeni,hisa za wamiliki pamoja na vitega uchumi.

Ikumbukwe bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania novemba mwaka jana lilipitisha sheria ya usimamizi wa huduma ndogondogo za fedha ya mwaka 2018 zinazoipa mamlaka Bot ya kusimamia biashara hizo nchini.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter