Home BIASHARA TAHA kupigania soko la matunda, mboga

TAHA kupigania soko la matunda, mboga

0 comment 167 views

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Wakulima wa Mboga, Matunda na Maua Tanzania (TAHA) Jackline Mkindi amesema kwa mwaka huu, taasisi hiyo imedhamiria kutosheleza soko la ndani la bidhaa zake na vilevile kufikia masoko ya kikanda, Afrika na Ulaya. Mkurugenzi huyo amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuongeza kuwa, licha ya changamoto zilizoikumba sekta ya kilimo mwaka jana, wawekezaji katika sekta hiyo waliweza kupata masoko ya kikanda na ya kimataifa.

Katika maelezo yake, Mkindi amesema kuwa kwa mujibu wa Ripoti ya East African Trade and Investment ya mwaka jana, imeripotiwa kuwa mauzo katika soko la kikanda yameendelea kuongezeka huku akieleza kuwa mwaka jana mauzo yaliongezeka kwa asilimia 11 wakati mwaka juzi, mazao yenye thamani ya Dola za Marekani 600,000 yaliuzwa katika soko la kikanda.

“Kwa hiyo utaona kati ya asilimia hizo 11, asilimia kubwa au 6 hivi inatokana na mazao ya mboga na matunda. Tanzania  imeongoza kwa mauzo katika masoko ya kikanda ya Afrika Mashariki”. Ameeleza Mkurugenzi huyo.

Pamoja na hayo, Mkindi amesema wanao mpango wa kuliteka zaidi soko la ndani japokuwa kuna kazi kubwa ya kuhamasisha watanzania kuwa na mazoea na kutumia mboga na matunda kama mlo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter