Home FEDHA Taasisi, madhehebu ya dini yafutiwa kodi ya pango la ardhi

Taasisi, madhehebu ya dini yafutiwa kodi ya pango la ardhi

0 comment 118 views

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ametangaza kuwa, kuanzia mwaka wa fedha 2018/2019, serikali imefuta kodi ya pango la ardhi kwa taasisi na madhehebu ya dini nchini. Lukuvi ametangaza hayo mkoani Mbeya wakati wa ibada ya kuwaweka wakfu viongozi wa Jumuiya Kuu ya Kanisa la Kibaptisti Tanzania (BCT) na kueleza kuwa, Rais Magufuli ameiagiza Wizara hiyo kutotoza kodi madhehebu ya dini kwa sehemu ambazo zimeandaliwa maalum kwa ajili ya ibada.

“Rais ameagiza kuanzia Julai mosi mwaka huu wa fedha madhehebu ya dini yasilipe kodi ya ardhi kwa maeneo ambayo huduma za maombi na ibada zinatolewa, hata hivyo msamaha huu hauhusu maeneo ambayo kuna miradi ya kuingiza fedha ambayo tunajua madhehebu mengi yameanzisha”. Amefafanua Lukuvi.

Waziri Lukuvi amesema kuwa tayari maagizo hayo yametolewa kwa makamishna wa ardhi wa kanda na mikoa pamoja na maofisa ardhi wa majiji, manispaa na halmashauri nchi nzima. Pamoja na hayo, Waziri huyo amewataka viongozi wa dini walio na migogoro ya ardhi kwenye maeneo ambayo wanatoa huduma kufika ofisini kwake jijini Dodoma.

“Wizara yangu imepewa jukumu la kutatua migogoro ya ardhi kabla ya mwaka 2020 na tusipotatua migogoro ya dini inaweza kupelekea uvunjifu wa amani nchini hivyo hatutaki kuifuga migogoro iliyopo”. Amesema Lukuvi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter