Home KILIMO Majaliwa asisitiza uhakiki, malipo wakulima wa korosho kukamilika

Majaliwa asisitiza uhakiki, malipo wakulima wa korosho kukamilika

0 comment 31 views

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amezitaka Wizara ya Kilimo pamoja na Bodi ya Mazao Mchanganyiko kuhakikisha wamekamilisha uhakiki na kuwalipa wakulima wote wa zao la korosho hadi kufikia Februari 5 mwaka huu. Waziri Mkuu amesema serikali inaendelea kufuatilia muelekeo wa mazao makuu ya biashara likiwemo la korosho kuanzia hatua ya uzalishaji hadi hatua ya masoko ili kuwapatia tija wakulima.

Akizungumza na wadau wa zao la korosho mkoani Mtwara, Waziri Majaliwa amesema serikali ilitoa nafasi kwa wafanyabiashara kufanya marekebisho ili kununua bidhaa hiyo kwa bei nzuri bila mafanikio hali iliyopelekea serikali kuchukua maamuzi ya kununua korosho zote.

Naye Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba amesema kuwa kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na timu ya uhakiki, kwa msimu wa 2018/2019 matarajio yalikuwa ni kuvuna tani 150,000 kutokana na kushuka kwa uzalishaji.

“Lakini kwa kazi nzuri iliyofanywa na timu nzima ya Wizara, wilaya na mkoa na timu ya uhakiki hadi sasa korosho tulizozipokea ambazo ziko katika maghala ni zaidi ya tani laki mbili”. Amesema Mgumba.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter