Home BENKI NMB yafuta tozo kunasa wateja

NMB yafuta tozo kunasa wateja

0 comment 91 views

Mkuu wa Kitengo cha Malipo na Akaunti wa NMB, Michael Mungure amesema benki hiyo imetangaza kufuta tozo mbalimbali kuanzia mwezi ujao ili kuharakisha kasi ya maendeleo ya mtu binafsi na taifa kwa ujumla. Mungure amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuongeza kuwa, baada ya kufanya tafiti za kina ili kujua kiini cha kutoongezeka kwa idadi ya wanaotumia huduma za kibenki, benki hiyo imeamua kuja na ‘free banking’.

Baadhi ya tozo zilizofutwa ni pamoja na ile ya kufungua akaunti kwa mteja mmoja mmoja (Individuals Account), ada ya kila mwezi (monthly maintenance fees), makato ya miamala (transactions fees) pamoja na yale ya kufufua akaunti ya zamani (dormant account).

“Hii tozo ya miamala tuliyofuta na ambayo itatumika kuanzia Februari mwaka huu ni ya kuhamisha fedha kutoka akaunti moja ya NMB kwenda akaunti nyingine ya NMB, lakini pia kutakuwa na huduma bure zilizotajwa hapo juu, pamoja kuuliza salio”. Amesema Mungure.

Naye Meneja Mwandamizi wa Bidhaa za Amana wa NMB. Stephen Adili, ametoa wito kwa watanzania kuchangamkia fursa ya kufutwa kwa tozo hizo kwa kufungua na kutumia huduma za NMB, ambazo zinapatikana kirahisi.

“Kuanzia sasa tunataka wateja wetu na watanzania kwa ujumla, waje wafungue akaunti kwa wingi na hakutakuwa na makato kama tulivyoainisha, fursa ambayo itaharakisha ustawi wa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla”. Amesema Adili.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter