Home VIWANDA Tanzania, Misri kujenga kiwanda

Tanzania, Misri kujenga kiwanda

0 comment 121 views

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesema Tanzania na Misri zimekubaliana kuanzisha kiwanda kikubwa cha nyama na mazao ya ngozi hapa nchini. Mpina amesema hayo jijini Dodoma baada ya kupokea wageni kutoka nchini Misri wakiongozwa na Waziri wa Kilimo wa nchi hiyo, Prof. Ezzaldin Aboussteit.

“Tunaenda kujenga kiwanda kikubwa cha kusindika nyama, cha kusindika ngozi, cha kusindika mazao ya ngozi, kiwanda ambacho hakipo katika nchi hizi zote za Afrika ya Mashariki na Kati”. Amesema Waziri Mpina.

Katika kikao hicho ambacho kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Abdallah Ulega, makatibu wakuu wa wizara pamoja na manejimenti, Mpina amemueleza Waziri huyo kutoka Misri kuwa, rasilimali zilizopo Tanzania ni salama na kusisitiza Wizara imekuwa ikifanya jitahada mbalimbali kuhakikisha samaki hawavuliwi kwa njia haramu ili kuhakikisha rasilimali hizo zinanufaisha viwanda vya ndani pamoja na wawekezaji walio na nia ya kuwekeza katika sekta hizo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter