Home FEDHABIMA TIRA yatoa mikataba ya Bilioni 1.44/-

TIRA yatoa mikataba ya Bilioni 1.44/-

0 comment 113 views

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini (TIRA) imetoa mikataba yenye thamani ya Sh. 1.44 bilioni kwa kampuni 23 kwa usambazaji huduma na uuzaji wa bidhaa nchini kwa mwaka 2017/2018. Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya mamlaka hiyo, wanufaika wa tenda hizo ni kampuni binafsi na zisizo binafsi, lengo likiwa ni kuendeleza soko la bima nchini.

Taarifa hiyo imetaja baadhi ya kampuni hizo kuwa ni Winglink Travel Limited, PUMA Energy Limitedd, Fein One Investment Limited, BM Printers Limited pamoja na Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA).

Katika mkataba huo, kampuni ya PUMA imepata Sh. 329.82 milioni kwa ajili ya kusambaza mafuta kwa wafanyakazi wa TIRA. Aidha, GPSA imepata sh. 245 milioni kwa ajili ya usambazaji wa vyombo vya moto.

Mojawapo ya nia ya mamlaka hiyo ni kukuza uchumi wa nchi ambapo hadi sasa, soko la bima hapa nchini lina makampuni yanayotoa bima aina zote 25, kampuni nne zinatoa bima za maisha, na moja inatoa bima za jumla na za maisha ambapo kampuni hizi zina takribani madalali 99. Pamoja na hayo, kuna kampuni za nje zinazotoa huduma za  bima 31 na madalali wa bima kutoka nje ni 41.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter