Home VIWANDA Gereza Kigoma kupewa kiwanda

Gereza Kigoma kupewa kiwanda

0 comment 115 views

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Viwanda na Biashara, kuhakikisha gereza la Kwitanga mkoani Kigoma linapatiwa kiwanda cha kisasa kwa ajili ya kukamulia mafuta ya mawese, ikiwa ni mchakato mojawapo wa serikali kufufua zao la michikichi hapa nchini. Majaliwa amesema hayo alipotembelea Gereza la Kwitanga ambapo alipata nafasi ya kukagua shamba la michikichi na vilevile kuzindua trekta.

Waziri Mkuu ameeleza kufurahishwa na mashine mpya ya kukamulia mafuta ya mawese katika gereza hilo ambapo mashine hiyo mpya itakuwa inatumia mota tofauti na hali iliyokuwa zamani wapolikuwa wanatumia mashine ya kusukumwa na mikono. Aidha, Majaliwa ameliagiza Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) kuimarisha teknolojia ya ukamuaji mafuta ili kusaidia kiwanda hicho kuzalisha kwa tija.

Kwa upande wake, Mkuu wa Magereza mkoani Kigoma, Leonard Burushi amesema uzalishaji wa mafuta umeongezeka kutoka pipa 63.4 kwa mwaka 2016/2017 hadi pipa 97 mwaka 2018/2019 huku zoezi la uvunaji bado likiendelea.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter