Home VIWANDA Kiwanda chahimizwa kuanza kazi mapema

Kiwanda chahimizwa kuanza kazi mapema

0 comment 157 views

Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda, amemtaka mmiliki wa kiwanda cha kuchakata nyama cha Elia Food Overseas kufanya jitihada zote ili kiwanda hicho kianze kufanya kazi Julai na si Oktoba, akidai kiwanda hicho kimekamilika kwa asilimia sabini na tano hivyo haiwezekani kianze kufanye kazi mwezi wa kumi. Waziri huyo amesema kufikia 2020, Longido itakuwa na viwanda vitatu ambavyo ni kiwanda cha ngozi, cha maziwa pamoja na hicho cha nyama.

Kakunda amemtaka mmiliki huyo kuwa na mahusiano mazuri na wanakijiji, Halmashauri na mkoa ili aweze kupata msaada pale atakapohitaji. Pia amesisitiza mmiliki huyo kutoa ajira asilimia 30 kwa wakazi wa kata hiyo na wilaya ili waweze kuwawezesha kiuchumi.

“Niseme tu si ombi kuhusu kutoa ajira, naagiza asilimia 30 ilenge wakazi wa eneo husika hata Longido ina wasomi wa kutosha wapeni ajira, ni aibu sana unafika kiwandani unauliza wafanyakazi wa Longido wako wangapi hakuna hata mmoja na kiwanda kipo hapa”. Amesema Waziri huyo

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kiwanda hicho Shabbir Virjee amesema watajitahidi kukamilisha ifikapo Julai mwaka huu na kumhakikishia Waziri kuwa kiwanda hicho kitatoa ajira zaidi ya 100 kwa vijana.

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter